Ile filamu iliyokuwa inaandaliwa na Msanii wako Hissani Muya almaarufu TINO, sasa imeshakamilika asilimia 100, Usiku wa tarehe 4 kuamkia tarehe 5 Filamu hii ilizinduliwa katika ukumbi wa Hotel ya Travertine Magomeni na Mheshimiwa mbunge Idd Azan. Sasa kinachosubiliwa na uwepo wake wa Filamu hiyo Sokoni na wewew ndugu Mtazamaji uende na kuchukua Nakala yako katika DVD Part One na Part two. "kuanzia tarehe kumi na Tano nadhani wakati wowote Filamu inaweza Kuwa sokoni" kama alivyosema Mkurugenzi wa Al-Riyamy Production ambao ndio wasambazaji wa Filamu hiyo. Kaa tayari kwa mkao wa kula
No comments:
Post a Comment