Tuesday, February 15, 2011

Chelsea Yanyosha Mikono juu..


Kocha Mkuu wa timu ya Mpira wa Miguu Uingereza Carlo Ancelotte jana alidhihirisha suala la wao kunyakua ubingwa msimu huu sasa ishakuwa ni suala la ndoto baada ya Mechi yao ya Jana dhidi ya Fulham kumalizika bila ya kufungana hivyo kuondoka na Pointi moja katika uwanja wa Craven Cottage.

"We have to come back quickly to get fourth place in the Premier League so we don't have time to think it is too much to be too far behind Manchester United. The most important thing is to finish in fourth place and I think we will be able to do this", akisema Ancelotte.


Chelsea sasa ipo nyuma ya vinara wa ligi hiyo Manchester United kwa Zaidi ya Pointi 12 na pointi 8 nyuma ya Arsenal ambao wanakama nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo yenye ushindani Barani Ulaya.


Haya sasa nadhani Mbio za Ubingwa wa ligi hiyo zimebaki mikononi mwa Manchester united na Arsenal na kwa Mbaali ikifuatiwa na Manchester City

Bodi ya Filamu yasimamisha utolewaji wa Filamu ya Shoga


Bodi kuu inayoshughulikia masuala ya Filamu Nchini wametoa tamko la kuizuia Filamu ya SHOGA iliyoandaliwa na Msanii Hissani Muya Almaarufu Tino isiingizwe sokoni mpaka ikaguliwe kuona kwamba inakidhi Mila, Desturi na Tamaduni zetu za Kitanzania Ndipo iruhusiwe kutoka.

Wale wapenzi ambao walikuwa wanasubiria kwa hamu kuona nini kilichoandaliwa ndani ya filamu hiyo wanaombwa kuwa wastahimilivu mpaka ukaguzi huo utakapokamilika ndipo filamu hiyo itakopoachiwa na kuingizwa sokoni

JInsi Filamu ya Shoga ilivyokuwa...

Emanuel Muyamba (Kulia) akijiandaa kuongea kitu kabla hajapata ruhusa toka kwa Muongozaji wa Filamu (Director) kulia kwake akiwa na Dada Kemmy (katikati) Otilia Joseph (aliyeshika kichwa) nae akiwa makini kusubiria maneno toka kwa Mchungaji.

Film Director Zavara (kushoto) akiwa makini kabla ya kuana kushoot, aliyeinama chini n Cameraman na Muhariri wa Filamu hii Yusuph Kissoky akiwa makini na Camera yake

Hissan Muya (Tino) akijiandaa kushoot



Charles Magari aliyecheza kama baba wa Tino ambaye amecheza kama shoga katika Filamu hiyo wakisubiria kitu...

Washika dau mbalimbali waliokuwepo Location nao wakifuatilia kwa makini

sasa Emanuel Muyamba Akifanya Vitu vyake

wakiweka Camera zao sawa









Thursday, February 10, 2011

Bongo Superstars Comedy, Yaendelea Kuykamua...

King Majuto (Kulia) akiwa na Kitale, wakiwa wanaendelea kushoot Comedy inayoitwa Alosto nje ya jiji la Dar-es-salaam ambako wamejichimbia

Comedian wakiendelea kukamua kama kawaida yao... hii nin ndani ya IN'YE

Wednesday, February 9, 2011

FIlamu ya Shoga yakaribia kuwa sokoni


Ile filamu iliyokuwa inaandaliwa na Msanii wako Hissani Muya almaarufu TINO, sasa imeshakamilika asilimia 100, Usiku wa tarehe 4 kuamkia tarehe 5 Filamu hii ilizinduliwa katika ukumbi wa Hotel ya Travertine Magomeni na Mheshimiwa mbunge Idd Azan. Sasa kinachosubiliwa na uwepo wake wa Filamu hiyo Sokoni na wewew ndugu Mtazamaji uende na kuchukua Nakala yako katika DVD Part One na Part two. "kuanzia tarehe kumi na Tano nadhani wakati wowote Filamu inaweza Kuwa sokoni" kama alivyosema Mkurugenzi wa Al-Riyamy Production ambao ndio wasambazaji wa Filamu hiyo. Kaa tayari kwa mkao wa kula

Avex Shot- Karibuni

Avex Shot ni Kampuni itakayokuletea mambo yote yahusuyo Sanaa mbalimbali ikiwa pamoja na Music, Filam nk. Pia itakujulisha juu ya mambo yote yahusuyo uandaaji wake, kuanzia Location hadi Post Production ya Film Mbalimbali kaa mkao wa kula...