Tuesday, February 15, 2011

Chelsea Yanyosha Mikono juu..


Kocha Mkuu wa timu ya Mpira wa Miguu Uingereza Carlo Ancelotte jana alidhihirisha suala la wao kunyakua ubingwa msimu huu sasa ishakuwa ni suala la ndoto baada ya Mechi yao ya Jana dhidi ya Fulham kumalizika bila ya kufungana hivyo kuondoka na Pointi moja katika uwanja wa Craven Cottage.

"We have to come back quickly to get fourth place in the Premier League so we don't have time to think it is too much to be too far behind Manchester United. The most important thing is to finish in fourth place and I think we will be able to do this", akisema Ancelotte.


Chelsea sasa ipo nyuma ya vinara wa ligi hiyo Manchester United kwa Zaidi ya Pointi 12 na pointi 8 nyuma ya Arsenal ambao wanakama nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo yenye ushindani Barani Ulaya.


Haya sasa nadhani Mbio za Ubingwa wa ligi hiyo zimebaki mikononi mwa Manchester united na Arsenal na kwa Mbaali ikifuatiwa na Manchester City

No comments: