Saturday, December 3, 2011

Filamu ya SHOGA YANGU sasa yatoka

Ile filamu ambayo ilikuwa ikisumbua masikio ya watu kwa kipindi kirefu na Serikali Kupitia bodi ya Filamu kuamua kuingilia kati na kusimamisha sasa imekamilisha taratibu zote na kuachiwa huru, na sasa ipo mitaani.


Filamu iliachiwa huru mwezi Mei ambapo baada ya kukaguliwa na kurekebishwa na kufuata matakwa yote ambayo serikali ilikuwa inataka yafanyike katika filamu hiyo, hivyo basi Jumatatu ya wiki hii tar 28 ndipo ilipoingia sokoni. Sasa unaweza ukaipata kwenye maduka yote ya kuuzia Filamu zetu Nchi nzima.

No comments: