Timu ya Mpira wa Miguu ya Chelsea yenye makazi yake katika jiji la London jumanne ya wiki hii walirudish matumaini ya kuendelea kugombania Kikombe cha ligi baada ya kuwafunga Mahasimu wao wanaoongoza ligi hiyo Manchester United katika mechi iliyofanyika katika uwanja wa Stamford Bridge (Darajani) kwa ushindi wa magori 2 - 1.
katika mechi hiyo ambayo Manchester United walikuwa wakwanza kupata gori kwa kupitia Mshambuliaji wake hatari Wyne Rooney ambaye alikanyaga mkwaju wa zaidi ya Yard 18 na kukwamisha Mpira wavuni. Baadaye Kipindi cha pili Chelsea walikuja juu na Kusawazisha goli la kwanza kwa kupitia beki wake wa kulia ambaye ni Mgeni David Luiz ambapo mkwaju huo ulimsababishia maumivu ya Mguu wa kushoto beki wa Man utd Patrick Evra ambaye alikuwa anajitahidi kuokoa mkwaju huo.
Baadaye Frank Lampard aliongeza gori la pili lililowapa ushindi kwa njia ya penati. Mpaka sasa chelsea inakamata nafasi ya nne ikiwa na pointi 48 nyuma ya Manchester utd pointi 12 na Mchezo mmoja mkononi. sasa chelsea inaomba Manchester utd ipoteze michezo mitatu kati ya michezo 11 iliyobakia ili iweze kumfikia kitu ambacho kwa sasa kinawezekana.
David Luiz akimkaba Wyne Rooney(Kulia)
No comments:
Post a Comment