Timu iliyoshiriki Mashindano ya Klabu Bingwa Barani Ulaya na kufikia hatua ya fainali mwaka jana Manchester United mwaka huu imeshindwa kuonesha cheche zake baada ya kutoka mapema zaidi katika mashindano hayo makubwa Barani Ulaya kwa Ngazi ya Klabu katika hatua ya Makundi (Mzunguko wa kwanza)
Magori yaliyowekwa kimiani na Marco Streller dakika ya tisa kipindi cha kwanza na Alexandre FREI katika dakika ya 82 na kuifanya FC Basel kuongoza kwa ushindi wa magoli 2 kwa 1 ambapo bao la Manchester united liliwekwa kimiani na Phil Jones kwa mpira wa kichwa, hivyo kuipa Basel tiketi ya kuingia katika hatua ya 16 bora.
Nao ndugu zao Manchester City wamejikuta wakiaga mashindano baada ya Ushindi wao kutegemea matokeo kati ya Villareal na Napoli ambapo napoli ilishinda kwa magori mawili kwa nunge na kumuacha City kwa point chache hivyo kujikuta Man City kuyaaga mashindano mapema pia.
hivyo basi wanakabumbu hao wote wawili wa jiji la manchester wanajikuta wakiangukia katika mashindano ya Kombe la Europa ambapo wataungana na Birmingham City, Stoke City, Liverpool na Totenham Hotspur.
Timu za London Arsenal pamoja na Chelsea zilifanikiwa kufuzu hatua ya 16 Bora juzi jumanne usiku baada ya kila mmoja kuongoza katika makundi yao.